Mwanamuziki wa nchini Marekani Janet Jackson
Janet Jackson amesema madaktari wake wamesema anahitaji kufanyiwa upasuaji haraka, hata hivyo hakueleza kuwa anasumbuliwa na kitu gani.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 49, amewaomba mashabiki wake wamuombee yeye, familia yake pamoja na kampuni yake katika wakati huu mgumu.
Janet Jackson alianza ziara yake hiyo Agosti Jijini Vancouver na alipangiwa kuifanya katika maeneo kadhaa ya Marekani, Canada na Ulaya Juni mwakani.