Motsepe ametambulisha kombe hilo jijini Dar es salaam amesema Msimu ujao watakuwa na timu 24 kwenye michuano ya African Football League nawatazipata kupitia ranki za CAF pamoja na mafanikio katika ligi za nyumbani.
"Nawashukuru viongozi wa timu zote nane zinazoshiriki michuano ya African Football League pamoja na zile 24 ambazo zitashiriki mwakani." Rais wa CAF, Patrice Motsepe.
Wakati huo huo Rais Motsepe amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan katika ikulu chamwimo Mkoani Dodoma