Monday , 21st Dec , 2015

Msanii Chege ambaye anafunga mwaka na video kubwa kabisa ya Sweety Sweety ft Runtown na Uhuru aliyoifanya huko Afrika Kusini chini ya Muongozaji Justin Campos, amesema kuwa muziki wa Bongo umekuwa mgumu, na hautaki tena vitu rahisi kama zamani.

Chege

Chege amesema kuwa, mabadiliko hayo ni changamoto kwa wasanii kuelekea mwaka 2016 akiamini kwa upande wake anamaliza mwaka vizuri kabisa na projekti hii mpya ambayo unaitazama sasa kupitia eNewz, (Sweety Sweety) kama anavyoeleza mwenyewe hapa.