Monday , 14th Dec , 2015

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye amesema, hatokuwa na msamaha na yeyote anayehusika katika kudhulumu haki za wanamichezo nchini kwani wao ndio chanzo cha kushusha michezo hapa nchini.

Nape amesema, kila mtu katika michezo anatakiwa kula kwa jasho lake na wale wanaohusika na kudhulumu haki za wanamichezo wanatakiwa kuondoka wenyewe na kama wasipoondoka atawaondoa kwani anawafahamu wote.

Nape amesema, katika vilabu kuna watu wanaojifanya viongozi wa michezo lakini hakuna mchezo hata mmoja wanaoufahamu na lengo lao kuingia katika michezo sio kukuza bali ni kudhulumu haki za wanamichezo na kuweza kushusha michezo.

Nape amesema, ili kuondoa migogoro katika Michezo ni lazima kuondoa walaji katika michezo kwani hawagombanii mafanikio katika michezo bali wanagombania ulaji katika michezo suala linalochangia michezo kufanya vibaya hapa nchini kutokana na migogoro.