Tuesday , 1st Dec , 2015

Nyota wa muziki Saraha ambaye yupo nchini Sweden aongea na eNewz kuhusu kuchaguliwa kwake na televisheni ya taifa kuwa mmoja wa washiriki wa tamasha kubwa la muziki lililobatizwa jina "Melodifestivalen 2016".

Nyota anayeuwakilisha muziki wa Bongofleva barani Ulaya Saraha

Saraha akiwa ni msanii anayeuwakilisha muziki wa Bongofleva barani Ulaya, atachuana na wanamuziki wakubwa barani Ulaya amesema kuwa tamasha hilo linahusisha Mashindano Maarufu na Makubwa ya Muziki nchini Sweden kwa mwaka 2016, ambapo mshindi ataiwakilisha Sweden katika Mashindano Makubwa ya nyimbo kwa nchi za Ulaya, "Eurovision Song Contest".

Hii itakuwa nafasi kubwa kwa Saraha kuutambulisha muziki wenye vionjo vya Kiafrika, yaani "Afro Pop" akiitangaza pia lugha ya Kiswahili kwa wapenzi wa Muziki wa Ulaya, ambapo mshindi wa mashindano haya anapata nafasi kubwa ya kuutangaza muziki wake.