Friday , 23rd Oct , 2015

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema sekta ya kilimo ikitiliwa mkazo ni nyenzo muhimu katika kutatua changamoto za kiuchumi na ajira nchini hususani kwa vijana.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua mavuno ya mahindi kutoka shambani kwake yaliyokusanywa nyumbani kwake Kibaoni wilayani Mlele,

Mh. Pinda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salama kwenye tukio la kuwekeana saini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Mh. Pinda ameongeza kuwa vijana wengi nchini hawana elimu ya kutosha ya kujiajiri wenyewe kutokana na kukosekana kwa misingi ya kujitegemea hivyo ni wakati sasa kwa vijana kutumika kwenye kuzalisha na kuongeza maendeleo ndani ya nchi kupitia sekta ya kilimo.

Waziri mkuu Pinda amesema wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ina wajibu wa kuwafuatilia vijana wote wanaochukuliwa na taasisi mbalimbali kwa malengo ya kuwasaidia.

Aidha ameongeza kuwa sekta ya kilimo ina uwezo wa kutoa ajira kwa vijana na kuwaingizia kipato cha kutosha hivyo wanapaswa kubadili mtazamo kuhusu ushiriki wao wa kilimo.