Sunday , 3rd May , 2015

Chama cha wamiliki wa daladala jijini Dar es salaam DARCOBOA kimesema hakina mpango wa kushiriki wala kuunga mkono mgomo wowote ule wa mabasi nchini.

Mwenyeekiti wa DARCOBOA Sabri Mabrouk

Chama cha wamiliki wa daladala jijini Dar es salaam DARCOBOA kimesema hakina mpango wa kushiriki wala kuunga mkono mgomo wowote ule wa mabasi nchini.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa DARCOBOA Sabri Mabrouk wakati akitoa msimamo wa wanachama wa DARCOBOA kuhusu tetesi za kuwepo kwa mgomo utakaoitishwa na chama cha wamiliki wa mabasi nchini Tanzania TABOA hapo kesho.

Kwa mujibu wa Mabrouk DARCOBOA imeanza kutekeleza matakwa ya serikali kuhusu maslahi ya madereva ili kuepusha adha na usumbufu wanaopata wananchi kutokana na migomo mbalimbali ya mabasi hapa nchini.

Amesema kuwa madereva wengi wanapenda kwenda njiani lakini wanaogopa vyombo vyao kuharibiwa kutokana na migomo ambayo hushinikizwa na baadhi ya madereva na wamiliki wake na kutaka wale wanaoweza wafanye safari zao kama ilivyo kawaida ili kusaidia wananchi huku malalamiko yao yakiendelea kutafutiwa ufumbuzi.