Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi nchini Tanzania UKAWA Bw. Freeman Mbowe
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mbowe amewataka wale wanaolalamika kwamba wameonewa kuacha kufanya hivyo kwa kuwa tathimini ilishafanyika na kuonekana kwamba wao hawana uwezo wala sifa za kupewa majimbo hayo..
Amesema katika UKAWA hakuna mtu atakayeonewa eti kwa sababu tu zisizo na msingi bali atachaguliwa kutokana na uwezo wake na matakwa ya wananchi hivyo wale wote ambao hawakuchaguliwa hawajaonewa bali uwezo wao umeenekana ni mdogo.
Aidha Mh. Mbowe ameongeza kuwa kesho kutakuwa na uchangishaji wa fedha katia ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kuwawezesha kuendelea na kupiga kampeni za urais kuweza kumalizia katika mikoa iliyobaki.
Pia Mh. Mbowe amesema ratiba ya Mh. Edward Lowassa kesho itaanza Gongolamboto na baadae mchana atahutbia Mbagala Zakiem na kumalizia katika ukumbi wa mikutano Mlimani City.