Wednesday , 19th Aug , 2015

Bodi ya ligi kuu nchini TPBL imetangaza ratiba ya ligi kuu ya soka Tanzania bara inayoanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu huku uwanja wa Karume ukitumika kwa ajili ya michuano hiyo na baadhi ya mechi kuchezwa mwishoni na katikati mwa wiki.

Akizungumza jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji wa TPLB Boniface Wambura amesema, uwanja wa Karume utatumiwa na timu ya JKT Ruvu katika mechi zake zote isipokuwa mechi za Simba na Yanga ambapo watatumia uwanja wa taifa huku mtibwa Sugar ikitumia uwanja wa Jamhuri badala ya Manungu Mkoani Morogoro.

Kwa upande wa shirikisho la soka Tanzania TFF imevisisitiza vilabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili kesho.