Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime.
Kauli hiyo inatolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David Misime wakati akizungumza na baadhi ya vikundi vya ulinzi shirikishi mkoani humo ambapo amesema dhamira ya jeshi hilo katika kuendelea kutoa mafunzo ya ulinzi shirikishi ili kupunguza uhalifu huku akitoa onyo kali kwa wahalifu wanaovitishia vikundi hivyo.
Kwa upande wake mratibu wa polisi jamii kutoka jeshi la polisi mkoa wa Dodoma afande Ally Bhujo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuvitumia vikundi hiyo katika kudumisha ulinzi hasa wakati huu ambapo taifa linakabiliwa na changamoto ya uchaguzi mkuu ujao.
Sebastian Sengolima ni moja kati ya mshiriki wa vikundi vya polisi jamii anaeleza mafunzo wanayoyapata na namna yanavyosaidia kupunguza uhalifu ikiwemo wizi wa mifugo.