Tuesday , 23rd Jun , 2015

Baada ya kushindwa kucheza ligi kuu soka ya Tanzania Bara msimu uliopita, Kiungo wa zamani wa Simba, Zahoro Pazzi amewaita mezani viongozi wa timu ya Mwadui FC ili kuangalia uwezekano wa kuvaa jezi zao msimu ujao.

Katika taarifa yake, Pazzi amesema, msimu uliopita alishindwa kucheza baada ya kuwa na matatizo na viongozi wa timu yake ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lakini anaamini kwa sasa yupo tayari kujiunga na timu yoyote hapa nchini itakayoonesha nia ya kumuhitaji.

Pazzia mesema, alienda Lupopo na kufanikiwa kucheza, lakini alikutana na vitendo viovu ambavyo ilibidi atoroke baada ya viongozi wa timu hiyo kughushi vitu vingi ikiwemo ITC.

Pazzi amesema, amesikia fununu za kutakiwa mwadui na kudai kuwa yupo tayari kukipiga na matajiri hao wa Shinyanga.