Monday , 28th Nov , 2016

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Yanga wameanza mazoezi leo chini ya Kocha Mkuu Mzambia George Lwandamina ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu pamoja na klabu bingwa Afrika.

Kutoka kushoto ni Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, George Lwandamina (Katikati) na Meneja wa Yanga Hafeedh Saleh wakiwa Uwanja wa Kurasini hii leo.

Akizungumza na Hotmix Michezo, kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Juma Mwambusi amesema, wameanza mazoezi na wanaangalia kama kuna umuhimu wa kuongeza wachezaji kwa ajili ya kuweza kuboresha kikosi zaidi.

Mwambusi amesema, wanaendelea kupanga mikakati na kocha Mkuu kwa ajili ya kuweza kuhakikisha wanaanza mzunguko wa pili vizuri na kuhakikisha wanatetea taji lao la ubingwa wa ligi pamoja na kufanya vizuri katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Baadi ya wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi leo Uwanja wa Kurasini jijini Dar es salaam.

 

Mwambusi amesema, kila kitu kipo katika mpangilio na wameona umuhimu wa kuweza kutetea taji hilo la ubingwa pamoja na kuweza kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika ushiriki wao uliopita katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Mwambusi amewataka mashabiki kuendelea kuipa sapoti timu ili kuweza kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.