
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema kuwa tayari baadhi ya vilabu vitaathilika na mpango huo na pia maoni ya wadau wengi yanaonyesha wazi kuwa mpango huo hauna manufaa kwa soka la kisasa
Aidha Mwakibinga amesema kuwa wadau wengi wanaamini uwepo wa wachezaji wa kigeni wenye sifa na ubora ni faida kwa taifa kwani wataleta ushindani kwa wachezaji wetu na wataongeza ujuzi na mbinu mpya kwa wachezaji wetu badala ya kukaa na kutumia wachezaji wa nyumbani pekee kitu ambacho hakitakua na faida katika soka hili la utandawazi.
