Wednesday , 4th Jul , 2018

Wakati dirisha la usajili kwa klabu ya Yanga likiendelea kimya kimya kama walivyodai, na kufanikiwa  kuleta takribani wachezaji 14 kutoka nje ya nchi waliokuja kufanya majaribio na kikosi hicho nchini, kati yao 8 wameondoka na 6 wakibakia.

Kikosi cha Yanga

Akizungumza na eatv.tv Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa kwa sasa wamebaki na wachezaji sita pekee huku wengine wakifeli mazoezi ambapo sasa watakuwa wanarejea makwao.

“Wachezaji waliofeli wameondoka kutokana na mchujo unaoendelea kwa ajili ya kupata wale wanaohitajika kwa ajili ya kukisuka upya kikosi kwaajili ya msimu ujao na michezo ya kimataifa”, amesema Saleh.

Yanga ilitangaza kuleta wachezaji 14 wa kimataifa kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu, Dismas Ten kwa ajili ya kufanya majaribio.  Kikosi hicho kipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.