Katika taarifa yake, Katibu mkuu wa TWA, Gola Kapipi amesema lengo la mashindano hayo ni kuongeza hamasa ya mchezo huo hapa nchini kama ilivyokuwa kwa michezo mingine.
Kapipi amesema, michezo itakayoshirikishwa katika mashindano hayo ni Wushu, Judo, Karate, Boxing na mingine inayohusiana na ngumi ili kutoa fursa kwa michezo mingine.

