Katibu Mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema, ni muda mchache umebaki kuanza kwa mashindano ya Olimpiki na kama chama kimeshapeleka majina mawili ya waogeleaji kwenda Shirikisho la mchezo wa kuogelea Duniani FINA na Julai 05 wanatarajia kupokea majibu kama wachezaji hao wanatakiwa kushiriki au hawatakiwi.
Namkoveka amesema, wachezaji hao wanaendelea na mazoezi katika nchi mbalimbali ambapo Hirary Hirary yupo mazoezini nchini Dubai, Magdalena Moshi anaendelea na mazoezi nchini Australia huku wakiwa wameongeza jina la muogeleaji mmoja Amary Gadial ambaye anaendelea na mazoezi nchini Canada.
Namkoveka amesema amesema, kikao hicho kitahusisha wajumbe wote wa kamati ya utendaji kutoka Tanzania bara na Zanzibar.