Sunday , 15th Feb , 2015

Timu ya Toto African ya jijini Mwanza imerejea rasmi katika ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo wa mwisho wa kundi B uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo mwingine wa funga dimba ya Ligi Daraja la Kwanza, timu ya Mwadui inayonolewa na kocha machachari kwa maneno Jamhuri Kihwelu ‘JULIO’ imeiadhibu timu ya Burkina Faso ya Morogoro mabao 4-3 katika mchezo uliopigwa katika machimbo ya Mwadui mkoani Shinyanga.

Mwadui imerejea ligi kuu ikiwa ni miaka 29 tangu ishiriki ligi hiyo mwaka 1986.

Kwa matokeo hayo Toto inayonolewa na John Tegete ambaye ni baba mzazi wa mchezaji wa Yanga Jerry Tegete imemaliza ikiwa na point 45 ikiwa nafasi ya Pili nyuma ya Mwadui iliyomaliza kileleni mwa kundi B na point 46.

Ligi hii iliyokuwa imetawaliwa na matukio kadhaa ya waamuzi kupigwa na michezo kuvunjika imehitimishwa leo kwa kutoa jumla ya timu 4 zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao (2015/2016) ambao utakuwa na timu 16 badala ya timu 14 kama ilivyo hivi sasa.

Timu zote zilizopanda daraja zimewahi kucheza ligi kuu, kwahiyo si timu ngeni kabisa.

Timu hizo ni African Sports ya Tanga, Majimaji ya Songea, Mwadui ya Shinyanga na Toto African ya Mwanza.