Thursday , 26th Jun , 2014

Uongozi wa chama cha masumbwi mkoa wa Tameke umeelezea kuridhishwa na mwitikio wa vilabu vya ngumi mkoani Temeke na hivyo kuwataka wadau kusaidia kuongeza hamasa katika michuano hiyo ambayo itakuwa na hadhi ya kimataifa

Mabondia wakichuana katika moja ya michuano ya ngumi Temeke.

Vilabu mbalimbali vya ngumi mkoa wa kimichezo wa Temeke vimeanza kuitikia wito wa kushiriki michuano ya klabu bingwa ya mkoa wa Temeke ambayo itashirikisha pia timu alikwa kutoka nje ya nchi ambazo ni Zambia, Kenya na Uganda

Mwenyekiti wa chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Temeke TEABA Said Omar 'Gogopoa' amesema mwitikio huo ni kutokana na vilabu vingi kutambua umuhimu wa michuano hiyo ambayo inahadhi ya kimataifa kutokana na TEABA msimu huu kuzialika timu zenye uzoefu toka nje ya nchi.

Aidha Gogo poa amewataka mabondia wakiwa katika vilabu vyao ambavyo vitashiriki michuano hiyo kujiandaa mapema na kufanya maandalizi ya nguvu na ya kutosha ili kuhakikisha wanabakisha medali nyingi iwezekanavyo hapa nchini,

Akimalizia Gogo poa amewaomba wadau na makampuni mbalimbali kugeukia mchezo wa masumbwi ili kuweza kuusaidia kwani ndio moja ya michezo ambayo siku za nyuma uliweza kuleta sifa kwa nchi yetu.