Sunday , 10th Jan , 2016

SIMBA SC imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo.

SIMBA SC imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo.

Shujaa wa Mtibwa Sugar FC leo alikuwa ni kiungo Ibrahim Rajab ‘Jeba’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45 akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa Peter Manyika baada ya shuti la mshambuliaji Hussein Javu anayecheza kwa mkopo kutoka Yanga SC.

Kwenye mchezo huo Simba ilionekana ikicheza bila ya kuelewana tofauti na mechi tatu za makundi walizocheza vizuri, huku Mtibwa ikitengeneza nafasi zaidi kwenye mchezo huo hadi kupata bao hilo.

Kwa matokeo hayo, Simba SC watapanda boti kesho mapema asubuhi kurejea Dar ea salaam, wakati Mtibwa Sugar itasubiri mshindi kati ya Yanga SC na URA ya Uganda usiku wa leo, ikutane naye katika fainali Jumatano.