
Edward Christopher aliyekuzwa na Simba lakini kwa sasa yupo Toto Africans ya Mwanza akifanya vizuri
Uongozi wa klabu ya Simba umekanusha kuwauza wachezaji wake walio kwa mkopo kwenye vilabu vingine, kama inavyopotoshwa na vyombo vingine vya habari.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema bado wachezaji hao wanamikataba na Simba, ila wapo kwenye vilabu hivyo kwa nia ya kupata uzoefu.
Poppe amesema wachezaji wa timu B, waliopelekwa kwa mkopo vilabu vingine, wanafatiliwa maendelea yao."Mfano kama yule kijana Mbaraka Yussuph, yupo Kagera Sugar, yule mchezaji yupo vizuri sana sasa hivi, na tulitaka kumrudisha, lakini yeye mwenyewe kaomba aendelee kupata uzoefu na sisi tumeona tumuongezee mkataba kwa sababu, tutamuhitaji baadae". amesema Poppe.