Sunday , 17th Jan , 2016

Wayne Rooney alifunga kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005,na kuisaidia Manchester United kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool jioni ya leo.

Rooney alifunga bao hilo dakika ya 78,kufuatia kichwa cha Maroune Felaini kugongwa mwamba na kurudi uwanjani kabla ya kufumua shuti na kuandika bao hilo pekee lilodumu hadi dakika ya 90.

Ushindi huo unaisogeza Manchester United hadi nafasi ya tano ikiwa inahitaji pointi mbili kuingia nne bora.

Liverpool itajilaumu yenyewe kwa kukosa nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza na kutokana na safu yake ya ushambuliaji kutokutulia wanapofika langoni,iliyokuwa ikiongozwa na Adam Lallana, Roberto Firmino, James Milner na Jordan Henderson.

Wachezaji mmoja mmoja waliokuwa wakionyesha uwezo binafsi,hasa Roberto Firmino kwa upande wa Liverpool na Antony Martial kwa upande wa Manchester United waliongeza burudani ya mchezo.