Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius anajiandaa kukata rufaa dhidi ya kesi inayomkabili ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mwezi Desemba mwaka uliopita mahakama ya juu nchini Afrika Kusini ilikubali rufaa iliwasilishwa na upande wa mashtaka ikitaka Pistorius apatikane na hatia ya mauaji, ambayo adhabu yake ni kali zaidi kuliko ya kuua bila kukusudia
Lakini katika kupinga hukumu hiyo hii leo mawakili wa Pistorius wamewasilisha maombi ya kutaka mahakama ya katiba kupitia tena hukumu hiyo.
Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 2013 baada ya kufyatua risasi kupitia mlango wa choo.

