Emmanuel Okwi
Kocha msaidizi wa The Cranes, Moses Basena alitangaza majina ya wachezaji 23, likiwamo jina la Okwi ambaye alishawahi kuchezea vialbu vya Tanzania Simba na Yanga, kipindi cha nyuma.
Basena amesema wamemwita Okwi kuwa Nahodha wa timu hiyo, ya Cranes kutokana na uzoefu wake katika uongozi, atasaidiana na Savio Kabugo wa Proline.
Hadi sasa mshambuliaji huyo, amepachika mabao 7, katika mechi 7 alizochezea Villa, tangu ajiunge na timu hiyo, mwezi Januari, akitokea klabu ya nchini Sweden SønderjyskE .
Kikosi hicho cha wachezaji wa ndani kinachojiandaa na mashindano ya CHAN, kimejumuisha baadhi ya sura mpya kama mlinzi wa Masavu, Brian Mukasa, Allan Drajua (Kirinya-Jinja S.S), Muhammed Ssekebba (Mbarara City ) Shafiq Kagimu (URA), Allan Anguy (Maroons) na Hudu Mulikyi (URA).

