Nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa FIFA wa dunia kwa mwaka 2015 na kukabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya 5.
Messi amepata tuzo hiyo katika hafla ya utoaji tuzo kwawanasoka bora zinazoto na shirikisho la soka duniani FIFA mjini Zurich nchini Uswis, akiwashinda Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Ureno, pamoja na Mbrazil Neymar anayekipiga katika klabu ya Barcelona.
Messi ameshinda wa kupata asilimia 41.33 dhidi ya Ronaldo aliyepata asilimia 27.76 huku Neymar akipata asilimia 7.86 ya kura zote.
Katika mwaka 2015 Messi amefanikiwa kuingoza klabu yake ya Barcelona kutwaa mataji matano, huku akiisaidia pia timu yake ya taifa kufika fainali ya Copa America.
Aliyeshinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kwa wanawake ni mchezaji wa timu ya taifa ya Marekani Carli LLOYD huku tuzo ya kocha bora wa mwaka imekwenda kwa kocha Barcelona Luis Enrique.
Enrique amepata asilimia 31.08 akimshinda Pep Guadiola aliyepata asilimia 22.97 na Jorge Sampaoli mwenye asilimia 9.46 ya kura zote.
Tuzo ya bao bora la mwaka imekwenda kwa Mbrazil Wendell Lira kwa bao la Machi11, 2015 akiwa na klabu ya Golanesia katika ligi ya Brazil.
Wendell amepata asilimia 46.7 dhidi ya Lionel Messi aliyepata asilimia 33.3 na Alessandro Florenzi aliyepata kura asilimia 7.1.
Kikosi bora cha mwaka ni :- e: Manuel Neuer, Thiago Silva, Marcelo, Sergio Ramos, Dani Alves, Andres Iniesta, Luka Modric, Paul Pogba, Neymar, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo.




