Thursday , 23rd Feb , 2017

Klabu ya Simba leo imemtangaza mshambuliaji wake Kimataifa Laudit Mavugo kuwa ndiye mchezaji bora wa mwezi Januari mwaka 2017.

Hiyo ni baada ya mashabiki wa Simba kupiga kura kupitia utaratibu ambao klabu hiyo imejiwekea ambapo kila mwezi mashabiki hupiga kura kupitia ukurasa wao wa facebook na kupendekeza mchezaji bora katika mwezi husika.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamemtaka mshambuliaji huyo kuendeleza moto huo huo siku ya Jumamosi ambapo timu yao hiyo itashuka dimbani katika uwanja wa Taifa kukipiga na watani wao wa jadi Yanga katika mechi ya marudiano katika Ligi Kuu Bara.

Hii ni sehemu ya maoni ya mashabiki hao