Wednesday , 29th Jun , 2016

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amesema, licha ya kupoteza michezo miwili mfululizo hawawezi kukata tamaa na matokeo yaliyopita yanabaki historia kwao.

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akitafuta njia ya kumtoka kiungo wa TP Mazembe, Nathan Sinkala

Niyonzima amesema, katika mpira kila timu inakuwa na malengo yake lakini hutokea makosa ambayo huja kuigharimu timu na kwa upande wao wanaagalia ni sehemu ipi ya kurekebisha.

Niyonzima amesema, wanajifunza kutokana na makosa hivyo katika maandalizi ya kuelekea katika mchezo ujao wanaangalia ni wapi walikosea ili kuweza kufanya vizuri.

Kwa upande mwingine Niyonzima amesema, mashabiki wanahitaji ushindi lakini hawawezi kuwaangusha mara zote kwani wanaendelea kujipanga kwa ajili ya ushindi.