Friday , 13th Apr , 2018

Martha Mwaipaja ambaye ni mwimbaji wa mziki wa injili amefunguka kuhusu tetesi za yeye kuwa na dharau pamoja na kujisikia ambapo amesema si kweli ila ana utaratibu wake ambao hauwezi kumfaa kila mtu.

''Ni kweli nimekutana na hizo tuhuma lakini kuna mazingira huwezi kuyakwepa haswa ukichagua kuwa mtu fulani lakini si dharau mimi ni mama wa kanisa kwahiyo huwezi tu kunipigia sijui twende wapi nikakubali'', amesema.

Aidha kupitia kipindi cha Kikaangoni Martha amesema wanaomtuhumu kuhusu kuwa na dharau ni waimbaji wenzake kwasababu yeye sio mtu wa kampani hivyo inakuwa ngumu kueleweka kwao.

''Kuna mwimbaji mmoja alinipigia simu akaniambia tunahitajika waimbaji mahali fulani nikamwambia mimi sitoweza nina ratiba nyingine, akanijibu tena nishaambiwa unadharau sana hutakubali'', ameongeza.