Saturday , 10th May , 2014

Rais wa TFF jamal malinzi anataraji kukutana na viongozi wa vilabu vyote vya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kuzungumzia mambo mbalimbali likiwemo la kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa na vilabu hivyo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi

Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi kesho saa 4 asubuhi katika ukumbi wa TFF anataraji kukutana na viongozi wa vilabu vya ligi kuu Tanzania bara na Ligi Daraja la Kwanza katika kikao maalumu alichokiitisha yeye mwenyewe

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kikao hicho kitawahusisha pia maofisa wa TFF na Bodi ya ligi na baadae maamuzi ya kikao hicho yatapelekwa katika kamati ya utendaji kwaajili ya kufanyia marekebisho kanuni za ligi baada kufanyika tathmini ya ligi hizo

Katika kuelekea kikao hicho baina ya Rais wa TFF na viongozi wa vilabu vya soka vya ligi kuu na daraja la kwanza Tanzania bara mmoja wa wadau wa soka nchini Paul Makoye ametoa ushauri kwa viongozi wa vilabu kuhakikisha wanakipitisha kipengele cha ongezeko la wachezaji wa kulipwa ama pengine wabaki watano kama ilivyo sasa.

Makoye amesema uwepo wa wachezaji wa kigeni una faida kubwa sana kwa soka letu na kimataifa kuliko kutaka kupunguza idadi ya wachezaji hao.