Thursday , 22nd Oct , 2015

Shirikisho la soka nchini TFF limesema malalamiko yanayotolewa na vilabu mbalimbali shiriki vya ligi kuu ya soka Tanzania Bara yanafanyiwa kazi kwa taratibu maalumu na mamlaka husika.

Afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto amesema, wanashirikiana na mamlaka mbalimbali kama vile watu wa ulinzi, usalama na hata Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa ajili ya kuhakikisha mpira unachezwa kwa usalama.

Kizuguto amesema, anaamini kila mwenye kazi yake anafanya ili kuhakikisha matatizo yote yanayotokea katika mechi mbalimbali za ligi kuu yanafanyiwa kazi.