Friday , 17th Jun , 2016

Ligi ya mpira wa wavu ya Mkoa wa Dar es salaam inatarajiwa kuendelea Julai 02 mwaka huu mara baada ya kusimamishwa ili kuvipa nafasi vilabu vya jeshi kushiriki mashindano ya jeshi.

Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa wavu mkoa wa dar es salaam DAREVA Yusuph Mkarambati amesema, mbali na vilabu vya jeshi pia zipo timu ambazo zinashiriki mashindano hayo ambazo pia zilipewa nafasi kwa ajili ya kushiriki mashindano ya UMISETA ambayo serikali imeyasitisha.

Mkarambati amesema, waliamua kutoa nafasi kwa vilabu hivyo kwani iwapo wangeendelea na mashindano kwa vilabu viwili kukosekana bado kungekuwa na muda wa kufidia.

Kwa upande mwingine Mkarambati amesema, Ligi ya vyuo imefikia katika hatua ya fainali ambayo imepangwa kupigwa Uwanja wa ndani wa Taifa wakati Ligi ya mkoa ikiendelea.

Mkarambati amesema, kwa upande wa Ligi ya mpira wa wavu wa ufukweni ya Mkoa inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwwzi Septemba mara baada ya kumaliza Ligi ya mkoa.

Mkarambati amesema, ligi ya mpira wa wavu wa ufukweni itakamilika mwezi Novemba ambapo ndiyo kalenda ya mwaka itakuwa itakamilika.