Friday , 21st Mar , 2014

Maandalizi ya mapema na kambi ndio jibu la medali

Kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa ya Tanzania Jonas Mwakipesile amesema kuwa dawa pekee ya kuondoa ama kufuta sababu za kufanya wana michezo nchini kutofanya vema katika michuano mbalimbali wanayoshiriki ni kufanya maandalizi ya mapema

Mwakipesile amesema kuwa kama timu itaandaliwa mapema ni wazi kutakua hakuna kisingizio cha kushindwa kufanya maajabu katika michuano mbalimbali

Mwakipesile amesema ana matumaini na kikosi chake ambacho ameanza nacho mazoezi na anauhakika kwa morali ya wachezaji na kujituma watafanya makubwa msimu huu.