Katibu wa JATA Innocent Malya amesema, wao kama chama walikosa fedha kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki mashindano ya kufuzu kushiriki Olimpiki lakini licha ya kukosa nafasi hiyo pia kunanafasi za upendeleo za ushiriki mashindano hayo na walipewa fomu ambazo walizijaza na kuziwasilisha Kamati ya Olimpiki nchini TOC lakini hawajapata majibu mpaka sasa.
Malya amesema, mpaka sasa wao kama viongozi wa chama wanashindwa kuwapa jibu sahihi wachezaji ambao wanatakiwa kuwa na maandalizi ya mapema kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yamebakisha miezi miwili ili kuanza.
Malya amesema, bado wanaendelea kusubiri majibu kutoka TOC kwani kwa muda waliojaza fomu mpaka sasa wangekuwa wameshapata majibu na kama maandalizi yangekuwa yameanza tangu muda.

