Beki wa kulia wa Leicester City akishangilia katika moja ya mechi za ligi kuu ya England
Nyota huyo mwenye umri wa miaka thelathini ameichezea Austria mechi sabini na nane ndani ya miaka kumi alipojumuishwa katika kikosi cha timu hiyo.
Akizungumza juu ya kustaafu kwake Fuchs amesema mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Iceland katika michuano ya mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa na anajisikia furaha kuwa miongoni mwa wachezaji walioaminiwa kutetea taifa lao uwanjani.
Nyota huyo alikuwemo kwenye kikosi cha Austria chenye nyota mahiri kama David Alaba wa Bayern Munich ya Ujerumani ilifungwa mabao mawili kwa moja na Iceland na kutupwa nje ya michuano ya mataifa ya Ulaya.
Fuchs alitua King Power Stadium akitokea Schalke 04 ya Ujerumani na kuisaidia Leicester City kufanya maajabu ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Engand .