Sunday , 10th Jan , 2016

Wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Pakistani ya mchezo wa kriketi, Salman Butt na Mohammad Asif wamerejea kwenye mchezo huo, baada ya kumaliza marufuku yao ya kutojishughulisha na mchezo huo kwa miaka 5.

Mohammad Asif na Salman Butt walifungiwa kifungo hicho kwa kufanya makusudi ya kupanga matokeo kwenye mechi ya Test dhidi ya Uingereza mwaka 2010.

Baada ya kumaliza kifungo hicho Butt amesema yeye ni kama mtu mpya kwa sasa na atajitahidi kurejea kwenye timu ya taifa ya Pakistan.

Mwezi wa Desemba mwaka uliopita Mohamed Amir ambaye naye alikuwa kwenye mkumbo huo aliachiwa kutoka marufuku ya miaka 5 na kurejeshwa kwenye timu ya taifa ambayo kwa sasa inajiandaa na michuano ya Twenty20 dhidi ya Newzealand wiki ijayo.