ameeleza hayo baada ya mashabiki wa mpira kusononeka kwa mchezo huo ambao baadhi yao walikuwa wanamlalamikia muamuzi kwamba alikuwa anawaonea Azam FC jambo ambalo likapelekea kupata matokeo mabaya wakiwa uwanjani kwao.
"Napenda kuwaomba radhi wapenzi wa mpira wa miguu na mashabiki wa timu ya Azam FC kwa mchezo tuliyocheza dhidi ya Yanga SC, ni sehemu ya mchezo lakini malengo tuliyokuwa nayo ni tofauti na matarajio tuliyokuja kuyapata baada ya mechi kumalizika", alisema Cheche.

Idd Cheche
Kwa upande mwingine, kikosi cha Azam FC teyari kimeshaanza safari yake ya kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Shupavu FC ambao umepangwa kuchezwa siku ya kesho (Jumanne) katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro saa 8:00 Mchana.


