Jinsi mila hii inavyofanyika
Mila hiyo inafahamika kama 'gukuna', ambayo hufanywa na shangazi au mama wa mtoto wa kike.
Mila hii ambayo inaonekana kuanza kutoweka kwa vijana wa sasa lakini inashamiri kwa wanawake ambao hawakuitekeleza wakiwa watoto, ikiwa na lengo hasa la kuongeza ashki wakati wa tendo la ndoa ili mwanamke aridhishwe zaidi.
Wanaume wa nchini Rwanda wamekaririwa wakisema kuwa ni muhimu kwa mwanamke kuridhishwa kwenye tendo la ndoa kuliko kuridhika wao pekee, na iwapo watashindwa kumridhisha basi hurudishiwa mahari yako au kunyang'anywa mke.