Gabo Zigamba
Gabo Zigamba amesema hayo kupitia 'Kikaangoni' inachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV na kusema kuwa marehemu Sajuki alikuwa mstari wa mbele kumpa nafasi na alimuamini kiasi cha kumshika mkono katika kila kazi mpaka yeye alipoanza kufanikiwa na kuanza kujulikana katika tasnia ni kutokana na jitihada za marehemu Sajuki.
"Marehemu Sajuki alikuwa na mchango mkubwa sana katika tasnia yangu, Mungu alimpa Sajuki baraka kwani bila yeye mimi nisingekuwa Gabo Zigamba leo, asilimia 75 ya umaarufu wangu leo hii ni kutokana na jitihada za Sajuki. Kwani alikuwa ananichukua na kunipa kipaumbele kwenye kazi zake, aliniamini mapema sana na kunipa nafasi mpaka nilipoanza kufanikiwa hivyo ana mchango mkubwa sana kwangu, huwa siwezi kumuongelea sana Sajuki kwani alikuwa mtu muhimu sana kwangu" Gabo Zigamba
Mbali na hilo Gabo Zigamba alisema kuwa pengo la marehemu Kanumba kwenye tasnia ya filamu litazibika tu ingawa anatambua kuna changamoto kubwa kuliziba pengo hilo ila anaamini litazibika tu siku moja.