Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Uwoya kuwa mchungaji, atangaza kuanzisha kanisa

Wednesday , 22nd Feb , 2017

Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.

Irene Uwoya - Msanii wa filamu

Kauli hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi alipokuwa akijibu maswali mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni

"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya

Uwoya pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya sanaa huwa inamtesa kiimani jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe anatubu kwa ajili ya mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .

Amesema katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa wanongea uongo na hata mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu ambavyo havimpendezi Mungu.

"Mimi nina hofu ya Mungu sana pia napenda kusali linapokuja suala la kazi yangu ukweli naona kama inanisumbua imani yangu kwa sababu katika uigizaji mambo mengi tunayoyafanya siyo ya kumpndeza Mungu lakini ndiyo kazi sasa, kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba msamaha mungu wangu ndiyo niendelee na kazi". Amesema Irene Uwoya.

Irene Uwoya akiwa Kikaangoni

Kwa waliotaka kujua kama Irene anatumia dawa za kulevya, amewajibu kuwa hatumii dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni mkristo na dini yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika ndoa za jinsia moja lakini pombe anakunywa

"Situmii dawa za kulevya lakini nakunywa bia, dini yangu haizuii kunywa, nina uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata mapadre kwenye dini yetu wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa"

Pia amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo fupi, ambapo amesema anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio 'allergy' na nguo ndefu, hivyo hawezi kuvaa nguo ndefu.

Mtazame hapa katika sehemu ya kipindi cha Kikaangoni kilichofanyika leo EATV......

 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea