Wednesday , 16th Jul , 2014

Baada ya kukubali kufanya kazi na msanii nyota wa nchini Uganda, Cinderella Sanyu aka Cindy, kundi la Urban Boys limekula shavu jingine la kufanya kolabo na nyota wa Nigeria Davido.

kundi la Urban Boys nchini Rwanda

Wakiwa wanatamba na video waliyoifanya na msanii Iyanya wa Nigeria kundi hilo maarufu la nchini Rwanda - Kigali wameanza kutengeneza kibao hicho kipya ambacho kitaachiwa muda si mrefu hewani.

Memba wa kundi hilo Humble Gizzo amesema walirekodi kipande cha wimbo huo mpya wakati wakiwa nchini Nigeria na wanatarajia kutua tena nchini humo kumalizia kazi hiyo.

Urban Boys wanatarajia pia kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya kolabo na kundi maarufu la Mafikizolo.