Akifunguka juu ya hilo, Sister Fay amesema kwamba hakuwahi kuwa na mahusiano na Holly Star, bali ilikuwa ni maigizo aliyokuwa akiyafanya, ambayo wengi waliamini ni kweli kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuigiza.
Sister Fay amesema kwamba ana uwezo mkubwa sana kwenye kuigiza, na ndio maana alifanikiwa kuwashawishi wengi kuhusu mahusiano yake na holly Star na kuonekana kama kuna ukweli.
Sister Fay anatoa siri
“Jamani mimi ni msanii, sasa hivi mnatakiwe mjue wasanii tupo, tunaweza kuigiza kitu mpaka mtu akaona ni real. Ile ilikuwa ni sanaa jamani, nafikiri kwa mara ya kwanza naiongea hapa, sikupenda kuiongea mwanzoni kwa sababu niliona ukiiongea mwanzoni siwezi kufikia malengo yangu, ile ilikuwa ni sanaa”, amesema Sister Fay.
Hivi karibuni iliaminika kuwa msanii huyo kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Holly Star hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa, baada ya picha kusambaa mitandaoni wakiwa na mavazi ya harusi.