Wednesday , 21st Oct , 2015

Msanii mkongwe wa muziki wa R&B R.

Msanii mkongwe wa muziki wa R&B R. Kelly, amefanya tamasha kubwa katika mji aliotoka wa Chikago, na kuanzisha kampeni ya kukusanya pesa ambazo angemsaidia mwalimu wake wa muziki alipokuwa akisoma.

R. kelly amesema ana deni kwa mwalimu huyo anayeitwa Lena McLin mwenye umri wa miaka 87, kwani ndiye aliyemfikisha alipo sasa kwa kumfundisha muziki, hivyo ameanzisha kampeni hiyo ambayo itamfanya aweze kulipia nyumba yake.

"Kwa mara ya kwanza nilipokutana nae, aliniambia unaenda kuwa mwimbaji mzuri na mwandishi mzuri, alinifundisha opera, classical, jazz na muziki wa dini, alisema wewe ni muziki, kila utakachojaribu utaweza, na hiyo ndio zawadi uliyonayo", alisema R.Kelly akimuelezea mwalim huyo.

Mwalimu huyo ambaye kwa zaidi ya miaka 36 amekuwa akitetea haki ya kuendelea kumiliki nyumba yake, hakutaka kumsumbua R. Kelly kwani aliamini ana mambo mengi anayoyafanya, lakini R. Kelly hakufurahishwa na hatua hiyo ya mwalimu wake kukaa kimya bila kumwambia chochote kuhusu tatizo lake.

"Nilimwambia ungeniambia tu, lakini alisema hakutaka kunisumbua kwa sababu alijua nina mambo mengi, nikamwambia umenifanya niwe mimi, mimi ni mtoto wako, ni jukumu langu kuwa kwa ajili yako kama ambavyo ulikuwa pale kwa ajili yangu, mimi ni kama mtoto mwengine kwa mama", alisema R. Kelly akiwa kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari mjini Chikago.