Sunday , 16th Aug , 2015

Burudani ya muziki na maonyesho ya Live, yameipamba siku ya jana katika onyesho la Party in The Park, likitawala nyuso za umati mkubwa uliohudhuria tukio hilo jana pale The Green Oysterbay Kenyatta Drive jijini Dar es Salaam.

wasanii wa kundi la Sauti Sol wakitumbuiza katika onyesho la Party In The Park jijini Dar es Salaam.

Kivutio kikubwa ikiwa kama ni burudani ya nyongeza ni onyesho la mrembo Feza Kessy ambaye kati ya burudani nyingine,akiwa sambamba na madansa wake aliweza kutumbuiza rekodi yake mpya ya Sanuka.

Kutoka nje ya mipaka ya Bongo, Beatenberg vilevile Black Motion, Sauti Sol, Ali Kiba, na Mafikizolo ni kati ya makundi yaliyotia nakshi burudani hiyo kwa midundo na shoo tofauti ya muziki.

Onyesho hilo la nguvu lilimalizwa na kundi la Mafikizolo ambalo sambamba na Bendi nzima na madansa wake walifanya jukwaa kuonekana halitoshi, vilevile mashabiki kukata kabisa kiu yao ya burudani.

Endelea kutazama EATV ambapo tutaendelea kukujulisha yaliyotokea katika onyesho hilo, tukiwa moja ya wadhamini wa nguvu kabisa wa burudani hiyo ya kukata na shoka.