Monday , 22nd Dec , 2014

Msanii wa muziki Nyota Ndogo, ambaye amekuwa ni moja kati ya wananchi ambao nyumba zao zimetakiwa kubomolewa Voi nchini Kenya kupisha ujenzi wa reli.

msanii wa muziki nchini Kenya Nyota Ndogo

Nyota amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, yupo katika mchakato wa kukamilisha nyumba yake mpya ambayo atahamia mwakani mwezi Machi akiweka wazi kuwa, amepata nguvu ya kusimamisha mjengo mwingine kutokana na malipo ya fidia ambayo ameyapata baada ya nyumba yake hii ya Voi kutakiwa kubomolewa.

Msanii huyu akiwa anawakilisha hisia za wengi, amesema kuwa kutakiwa kuhama katika nyumba hii ni kitu ambacho kilimuuma na kumliza sana, hasa akikumbuka jitihada zake za kujenga mpaka kukamilisha na hatimaye kuanza maisha ndani yake.