Wednesday , 22nd Jun , 2016

Msanii wa kitambo kidogo aliyepata mafanikio na kupotea kwenye game na kusikika ameibukia katika machimbo ya madini amerudi tena kwenye game la bongo fleva chini ya Said Fela.

FEROOZ

Enewz imepiganae stori kutaka kujua ni vipi ameacha biashara za madini.......

Ferooz ameiambia Enews kwamba amerudi rasmi kwenye game na amejipanga vizuri sana yeye pamoja na menejiment yake ambapo kwa sasa amesema yupo chini ya Mkubwa Fella na watu wategemee mambo mazuri kutoka kwake.

Hata hivyo Ferooz amesema hajatoka katika biashara zake za madini na bado atakuwa akienda mkoani Arusha mara moja moja kuangalia dili zake nyingine nje ya muziki kwa kuwa yeye ana dili zake nyingi Arusha.

Ferooz anasema hajali maneno ya watu yanayoongelewa kwamba sasa hivi anatumia madawa ya kulevya na kuvuta bangi, anasema anamshukuru Mungu kwamba katika matusi yote hayo hajawahi kuhusishwa na mambo ya ushoga.