Thursday , 15th May , 2014

Msanii wa Muziki Diamond Platnumz, ameingia kwa kishindo katika jukwaa la burudani la Kimataifa rasmi baada ya kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo kubwa kabisa duniani za burudani zinazotolewa na kituo kikubwa cha Televisheni cha Marekani.

Diamond Platnumz, anakuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kuingia katika kinyang'anyiro cha tuzo hizi kwa mwaka huu, akiwa katika kipengele cha msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika kupitia ngoma yake iliyofanya vizuri sana na “My Number One”, ambapo tayari mastaa na wadau mbalimbali wa muziki wametoa pongezi na sapoti ya kutosha katika kufanikishaushindi kwa msanii huyu.

Katika kipengele hiki, Diamond anapambana na wasanii wengine wakali kutoka Afrika, akiwepo Toofan kutoka Togo, Tiwa Savage kutoka Nigeria, Sarkodie kutoka Ghana, Davido wa Nigeria na kundi la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini.

Tuzo hizi zitafanyika tarehe 29 mwezi Juni mwaka huu, na kushereheshwa na mchekeshaji maarufu duniani, Chris Rock.