Tuesday , 28th Aug , 2018

Msanii kutoka 'Green City' akiwakilisha kundi la 'The Amazing', Izzo Bizness amewataka mashabiki na wadau wa muziki nchini, kuacha kulalamika bila ya kuwa na sababu za msingi kuhusu kubadilika muziki wa hiphop.

Izzo Bizness

Izzo ameeleza hayo alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wadau hao, wakidai wasanii wa sasa hawafuati misingi ya uimbaji wa hiphop na badala yake wamekuwa wakifanya hiphop laini ili waweze ku-trend mitandaoni.

"Hakuna hiphop ngumu, watu wanapaswa wafahamu hilo. Hiphop ni muziki ambao unaleta hofu kwenye jamaa na mimi huo muziki ninao means ninaimba kila leo. Watu wasiwe wanalalamika tu, wawe na sababu za msingi", amesema Izzo.

Pamoja na hayo, Izzo ameendelea kwa kusema "hiphop sio kwamba hailipi sema tu ni vile watu au wasanii jinsi wanavyoibeba na kutoa nyimbo za kawaida sana ndio maana hawapati faida na wanachokifanya".

Kauli hizo za Izzo Bizness zimekuja baada ya kuonekana muziki wa hiphop nchini kama umeyumba kwa kiasi fulani, kwa kile kinachoonekana kwa wasanii wa kurap kuimba nyimbo laini na kuacha zile njia za msingi ambazo zimekuwa zikizungumzia changamoto mbalimbali za maisha.

Msikilize hapa chini akizungumza zaidi.