Wednesday , 6th Jan , 2016

Kauli ya rapa Baghdad juu ya kuchukuliwa aliyekuwa mpenzi wake na Mesen Selekta, imeibua kutokuelewana tena kati yao hasa kutokana na Mesen kutokufurahishwa na taarifa hiyo kwa madai kuwa inaathiri familia yake akiwa baba wa mtoto mmoja sasa.

msanii wa muziki nchini Mesen Selekta

Mesen Selekta ameeleza kwa undani kuwa, kauli ya Baghdad haileti picha nzuri kwa nafasi yake sasa, mwanadada ambaye anamtuhumu kumuibia akiwa alimfuata Mesen kwa kumuelewa mwenyewe kutokana na Baghdad kutokuwa na mvuto kipindi cha nyuma akiwa na umbo nene.