Wednesday , 19th Aug , 2015

Msanii wa kizazi kipya Mdoti ambaye ametoa kazi yake ya kwanza 'Penzi la Dhati' itakayotambulishwa rasmi EATV Ijumaa hii amesema kuwa nafasi yake kama msanii chipukizi ni kufanya muziki unaoendana na mahadhi ya nyumbani.

Msanii wa kizazi kipya Rashid Shaban aka Mdoti

Rashid Shaban a.k.a Mdoti ameongea na eNewz kuwa hii ni kazi ambayo imefanyiwa kazi na producer mahiri nchini Issa Touch na pia ameweka wazi kuhusiana na jina lake hilo la Mdoti huku akiwasihi mashabiki na wadau kuonesha umoja katika kuinua kazi za wasanii chipukizi nchini.