Wednesday , 6th May , 2015

Rapa wakazi, msanii ambaye pengine ndiye anayeshikilia rekodi kwa kupata nafasi ya kukutana na mastaa wengi na wakubwa wa muziki duniani, afafanua sababu ya picha hizo ambazo zimeleta gumzo kwa mashabiki wake.

rapa Wiz Khalifa akiwa na msanii wa bongofleva Wakazi

Staa huyo ameamua kuongea na E-Newz huku akitolea ufafanuzi ni kwanini watu wamekuwa wakiona picha zake tu na mastaa hao, na si kusikia kolabo kati yake na wao.

Rapa huyu ambaye sehemu ya maisha yake amekuwa akiishi nchini Marekani amesema kuwa, nafasi ya kukutana na ma "Supa Staa" hao wa dunia, imemuwezesha kujifunza mambo mengi na kujitengenezea nafasi ambazo zimemfikisha mpaka alipo sasa kisanaa, kama anavyosema hapa.