
Kundi la The Quest Crew, ambalo limefanikiwa kutinga tano bora ya usaili wa Dance100 Don Bosco Upanga Dar es salaam.
Jaji Super Nyamwela amesema hamasa imezidi kuongezeka katika shindano hilo kutokana na vijana kutambua umuhimu wa shindano pamoja na zawadi iliyopo ambapo kwa sasa mshindi kunyakua shilingi milioni 7.
''Makundi mengi yamejitokeza na hii inaashiria kwamba uelewa wa shindano ndani ya jamiii unazidi kuongezeka , ndiyo maana kuna makundi mengi yametoka mikoani kuja kuonesha vipaji jambo ambalo ni jema ili waweze kutambulika na kupewa nafasi kulingana na ubunifu na uwezo wao''Asmesema Jaji Nyamwela
Baada ya vijana kuonyesha uwezo wao kwa kila kundi kuonyesha utofauti na jingine makundi ambayo yameweza kufanikiwa kushinda katika usaili wa leo ambayo ni J Combat Crew, The Heroes Crew, The Quest Crew, TWC na Wazawa Crew.
